UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015

ISBN: 978-1-4769-2790-9

Category: Current Events

Keywords: TANZANIA, LOWASSA, MAGUFULI, CCM, UKAWA, UCHAGUZI, SIASA

Published: 10/04/2015

Views: 906

Words: 24,668

Rating:

UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015

MAGUFULI vs LOWASSA

By

Kitabu hiki kinahusu Uchaguzi Mkuu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, utakaofanyika Oktoba 25, 2015. Kinachambua chaguzi kuu zilizopita, na mazingira ya sasa ambapo uchaguzi huu unafanyika. Kadhalika, kitabu hiki kinachambua michakato ya kambi kuu mbili katika kupata wagombea wake wa urais. Kambi hizo ni Chama tawala CCM na UKAWA, na wagombea wao Dkt John Magufuli (CCM) na Edward Lowassa (UKAWA). Katika uchambuzi huo, kitabu kinaangalia nafasi na vikwazo kwa kila kambi na mgombea wake. Lengo kuu la kitabu hiki ni kuwapa Watanzania uelewa wa kutosha kuhusu zoezi zima la Uchaguzi Mkuu, sambamba na kuzielewa kambi hizo kuu na wagombea wake, ikitarajiwa kuwa itawasaidia kufanya maamuzi sahihi siku ya kupiga kura

Kbook iPad Reader UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015

Read it on any Device that supports ePub

Buy to read on eBook Tablet

$2.49

Kbook Mobile Reader

About the Author

Oct 04, 2015

Mwandishi wa kitabu hiki, Evarist Chahali, ni Mtanzania mwenye makazi yake jijini Glasgow, Uskochi, na anajitambulisha kama mwanaharakati wa mtandaoni (e-activitist) katika masuala ya haki za kijamii. Ni mhitimu wa Shahada ya kwanza katika Sosholojia (BA in Sociology) aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Shahada ya Uzamili katika Stadi za Vita (Master of Letters in War Studies) na Shahada ya Uzamili katika Utafiti wa Siasa (Master of Research in Political Research) alizopata katika Chuo Kikuu cha Aberdeen, Uskochi, ambapo bado anaendelea na Shahada ya Uzamifu katika Stadi za Siasa (PhD in Political Studies – Part-Time).
Kwa zaidi ya miaka 10, amekuwa akiandika makala katika magazeti mbalimbali nchini Tanzania, ambapo huko nyuma aliandikia magazeti ya ‘Kulikoni’ na ‘Mtanzania,’ na kwa sasa ni mwandishi wa makala katika gazeti la kila wiki linaloongoza nchini Tanzania, la ‘Raia Mwema. Kadhalika, mwandishi anamiliki blogu ya ‘Kulikoni Ughaibuni’ iliyoanzishwa mwaka 2006.

Awali, mwandishi alikuwa Mwalimu katika Shule ya Sekondari ya Ecknforde, Tanga, Tanzania kabla ya kujiunga na utumishi serikalini katika Ofisi ya Rais wa Jamhuri wa Munngano wa Tanzania. Hivi sasa, licha ya kuendelea na masomo yake ya Shahada ya Uzamifu (part-time) anajihusisha ushauri wa masuala ya intelijensia (intelligence consultancy).

> More about the Author

Recommended Books Arrow

Similar Books

Discussion - 3 comments

About Kbuuk

  • Our Story

    Inspired by the past and excited for the future, Kbuuk charges ahead.

  • Our Manifesto

    Kbuuk empowers authors worldwide. Come see what empowers us!

  • The Team

    Meet the Team. Find out who is behind every line of code.

Find out first:

Kbuuk Reader