Dokta John Magufuli

ISBN: 978-1-4769-6966-4

Category: Political,  Africa

Keywords: Tanzania, Politics, Africa, Magufuli, Lowassa, CCM, UKAWA

Published: 12/31/2015

Views: 833

Words: 24,765

Rating:

Dokta John Magufuli

Safari ya Urais, Mafanikio Na Changamoto katika Urais wake

By

Kitabu hiki ni toleo la pili la kitabu cha ‘Uchaguzi Mkuu Tanzania 2015: Magufuli vs Lowassa,’ ambacho kilijadili kwa kina kuhusu uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani nchini Tanzania, uliofanyika Oktoba 25 mwaka 2015. Kilichonisukuma kuandikia toleo hili la pili ni pamoja na ukweli kwamba toleo la kwanza lilitoka takriban wiki mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu na hivyo kuwanyima fursa wasomaji wengi watarajiwa. Kadhalika, nimeonelea kuna haja ya kufanya tathmini ya uchaguzi huo ulioshuhudia mgombea wa chama tawala, CCM, Dkt John Pombe Magufuli akiibuka mshindi na kuapishwa kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kbook iPad Reader Dokta John Magufuli

Read it on any Device that supports ePub

Buy to read on eBook Tablet

Buy Now  > $2.49

Kbook Mobile Reader

About the Author

Oct 04, 2015

Mwandishi wa kitabu hiki, Evarist Chahali, ni Mtanzania mwenye makazi yake jijini Glasgow, Uskochi. Ni mhitimu wa Shahada ya kwanza katika Sosholojia (BA in Sociology) aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Shahada ya Uzamili katika Stadi za Vita (Master of Letters in War Studies) na Shahada ya Uzamili katika Utafiti wa Siasa (Master of Research in Political Research) alizopata katika Chuo Kikuu cha Aberdeen, Uskochi, ambapo bado anaendelea na Shahada ya Uzamifu katika Stadi za Siasa (PhD in Political Studies – Part-Time).
Kwa zaidi ya miaka 10, amekuwa akiandika makala katika magazeti mbalimbali nchini Tanzania, ambapo huko nyuma aliandikia magazeti ya ‘Kulikoni’ na ‘Mtanzania,’ na kwa sasa ni mwandishi wa makala katika gazeti la kila wiki linaloongoza nchini Tanzania, la ‘Raia Mwema. Kadhalika, mwandishi anamiliki blogu ya ‘Kulikoni Ughaibuni’ iliyoanzishwa mwaka 2006.
Awali, mwandishi alikuwa mwalimu katika Shule ya Sekondari ya Ecknforde, Tanga, Tanzania kabla ya kujiunga na utumishi serikalini katika Ofisi ya Rais wa Jamhuri wa Munngano wa Tanzania. Hivi sasa, licha ya kuendelea na masomo yake ya Shahada ya Uzamifu (part-time) anajihusisha ushauri wa kitaalamu katika masuala ya intelijensia na usalama (intelligence and security consulting), mikakati ya siasa (political strategy consulting) na mahusiano na mawasiliano ya kimkakati (International PR and strategic communications), akiwa mwanzilishi na mmiliki wa kampuni ya ushauri wa kitaalam ya AdelPhil Consultancy iliyopo Glasgow, Uskochi.

> More about the Author

Recommended Books Arrow

Similar Books

Discussion - 8 comments

About Kbuuk

  • Our Story

    Inspired by the past and excited for the future, Kbuuk charges ahead.

  • Our Manifesto

    Kbuuk empowers authors worldwide. Come see what empowers us!

  • The Team

    Meet the Team. Find out who is behind every line of code.

Find out first:

Kbuuk Reader