Makala za Evarist Chahali Zilizovuma Magazetini

ISBN: 978-1-4769-8703-3

Category: Political,  Reference,  Essays & Letters

Keywords: Tanzania, Chahali

Published: 01/31/2016

Views: 498

Words: 48,634

Rating:

Makala za Evarist Chahali Zilizovuma Magazetini

Toleo la Kwanza

By

Kitabu hii ni toleo la kwanza la mkusanyiko wa makala zangu mbalimbali katika magazeti ya 'Kulikoni,' 'Mtanzania,' na 'Raia Mwema' nilizoanza kuandika tangu mwaka 2006.

Makala hizo zinatoa picha ya yaliyojiri katika kipindi cha miaka hiyo 10 yaani 2006 hadi mwaka huu 2016. Ikumbukwe kuwa takriban nusu ya kipindi hicho, uwepo wa vyombo mbalimbali mtandaoni ulikuwa hafifu, na mitandao ya kijamii haikuwa na umaarufu ilionao sasa. Kwahiyo makala hizo zinamsaidia msomaji kufahamu masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika kipindi hicho, ambayo kama kawaida yangu, niliyaandika katika hali ya maongezi na wasomaji wa makala hizo (conversation style).

Ni matumaini yangu kuwa kitabu hiki kitakuwa na manufaa kwa wasomaji hususan kuelewa wapi tulipotoka, tullipo na tunedako, kama taifa.

Kbook iPad Reader Makala za Evarist Chahali Zilizovuma Magazetini

Read it on any Device that supports ePub

Buy to read on eBook Tablet

$2.49

Kbook Mobile Reader

About the Author

Oct 04, 2015

Mwandishi wa kitabu hiki, Evarist Chahali, ni Mtanzania mwenye makazi yake jijini Glasgow, Uskochi, na anajitambulisha kama mwanaharakati wa mtandaoni (e-activitist) katika masuala ya haki za kijamii. Ni mhitimu wa Shahada ya kwanza katika Sosholojia (BA in Sociology) aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Shahada ya Uzamili katika Stadi za Vita (Master of Letters in War Studies) na Shahada ya Uzamili katika Utafiti wa Siasa (Master of Research in Political Research) alizopata katika Chuo Kikuu cha Aberdeen, Uskochi, ambapo bado anaendelea na Shahada ya Uzamifu katika Stadi za Siasa (PhD in Political Studies – Part-Time).
Kwa zaidi ya miaka 10, amekuwa akiandika makala katika magazeti mbalimbali nchini Tanzania, ambapo huko nyuma aliandikia magazeti ya ‘Kulikoni’ na ‘Mtanzania,’ na kwa sasa ni mwandishi wa makala katika gazeti la kila wiki linaloongoza nchini Tanzania, la ‘Raia Mwema. Kadhalika, mwandishi anamiliki blogu ya ‘Kulikoni Ughaibuni’ iliyoanzishwa mwaka 2006.

Awali, mwandishi alikuwa Mwalimu katika Shule ya Sekondari ya Ecknforde, Tanga, Tanzania kabla ya kujiunga na utumishi serikalini katika Ofisi ya Rais wa Jamhuri wa Munngano wa Tanzania. Hivi sasa, licha ya kuendelea na masomo yake ya Shahada ya Uzamifu (part-time) ni mwanzilishi na mmliki wa kampuni ya AdelPhil Consultancy inayojihusisha na ushauri wa kitaalamu wa masuala intelijensia (intelligence consultancy), mikakati ya siasa (political strategy) na mahusiano na mawasiliano ya kimkakati (International PR and strategic communications)

> More about the Author

Recommended Books Arrow

Similar Books

Discussion - 0 comment

About Kbuuk

  • Our Story

    Inspired by the past and excited for the future, Kbuuk charges ahead.

  • Our Manifesto

    Kbuuk empowers authors worldwide. Come see what empowers us!

  • The Team

    Meet the Team. Find out who is behind every line of code.

Find out first:

Kbuuk Reader