Shushushu

ISBN: 978-1-4769-3228-6

Category: Political,  Reference

Keywords: Tanzania, Intelligence, Security, Spying, Espionage, CIA, Usalama wa Taifa

Published: 02/13/2016

Views: 1070

Words: 33,201

Rating:

Shushushu

Afisa Usalama wa Taifa ni mtu wa aina gani, anafanya nini?

By

Kitabu hiki ni matokeo ya mfululizo wa makala (series) nilizozichapisha katika blogu yangu ya ‘Kulikoni Ughaibuni’ kuhusu fani ya Uafisa Usalama wa Taifa (ushushushu). Kutokana na makala hizo kuonekana kuwavutia wasomaji wengi, niliona umuhimu wa kuzikusanya pamoja na kutengeneza kitabu hiki.
Kadhalika, binafsi niliwahi kuwa Afisa Usalama wa Taifa huko Tanzania, kazi niliyoifanya kwa miaka 13. Na kwa vile ni maafisa usalama wachache mno, walio kazini au nje ya kazi, wenye fursa ya kuelezea kuhusu fani hiyo nyeti, wazo la kuandika kitabu hiki linakidhi haja hiyo.
Ukosefu wa machapisho kuhusu taaluma hiyo nyeti kumechangia sana mkanganyiko katika jamii kuhusu ushushushu na mashushushu huku baadhi wakiamini kwa dhati kabisa kuwa taaluma hiyo inahusika na ‘mambo mabaya tu,’ kama vile kuuwa watu wasio na hatia, umumiani (kunyonya damu kama ‘vampires,’) na hisia potofu kama hizo.
Kwahiyo kitabu hiki, bila kukiuka kanuni na sheria za usiri zinazotawala taaluma hiyo, kinajaribu kufungua ukurasa mpya, angalau kwa huko nyumbani, kutoa picha ya jumla kuhusu taaluma hiyo muhimu mno kwa usalama na ustawi wa taifa letu, sambamba na kuelezea kwa undani mchango muhimu wa mashushushu kwa usalama wa taifa letu, ikiwa ni pamoja na kubainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili, na kutoa mapendekezo ya kuzikabili.
Kwa ‘nchi za wenzetu,’ mashushushu wastaafu wamekuwa vyanzo vikuu vya uelewa kuhusu fani hiyo nyeti ambapo wamekuwa wakiandika vitabu mbalimbali, ilhali wengine wakishirikiana na sekta ya filamu katika utengenezaji wa filamu zinazohusu ushushushu. Kwa bahati mbaya (au pengine kwa makusudi tu), kwetu ile kuzungumzia tu jambo lolote linalohusu ushushushu ni kitu adimu mno. Kasumba hiyo imeawaathiri hata wanataaluma ambao hawajawahi kujihusisha kufanya tafiti au kuandika machapisho ya kitaaluma kuhusu fani hiyo. Uhaba wa ‘references’ unatoa kisingizio kizuri kwa wasomi wetu ‘kupuuzia’ mada hiyo muhimu.
Kimsingi, taaluma ya ushushushu inatawaliwa na usiri, na mengi ya yanayohusiana na taaluma hayo yanabaki kuwa siri. Hata hivyo, kuna maelezo ambayo yapo wazi japo inahitaji uelewa wa aina flani kuchora mstari kati ya kipi ni siri na kipi ni ruksa kuwa hadharani.

Kbook iPad Reader Shushushu

Read it on any Device that supports ePub

Buy to read on eBook Tablet

$2.99

Kbook Mobile Reader

About the Author

Oct 04, 2015

Mwandishi wa kitabu hiki, Evarist Chahali, ni Mtanzania mwenye makazi yake jijini Glasgow, Uskochi. Ni mhitimu wa Shahada ya kwanza katika Sosholojia (BA in Sociology) aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Shahada ya Uzamili katika Stadi za Vita (Master of Letters in War Studies) na Shahada ya Uzamili katika Utafiti wa Siasa (Master of Research in Political Research) alizopata katika Chuo Kikuu cha Aberdeen, Uskochi, ambapo bado anaendelea na Shahada ya Uzamifu katika Stadi za Siasa (PhD in Political Studies – Part-Time).
Kwa zaidi ya miaka 10, amekuwa akiandika makala katika magazeti mbalimbali nchini Tanzania, ambapo huko nyuma aliandikia magazeti ya ‘Kulikoni’ na ‘Mtanzania,’ na kwa sasa ni mwandishi wa makala katika gazeti la kila wiki linaloongoza nchini Tanzania, la ‘Raia Mwema. Kadhalika, mwandishi anamiliki blogu ya ‘Kulikoni Ughaibuni’ iliyoanzishwa mwaka 2006.
Awali, mwandishi alikuwa mwalimu katika Shule ya Sekondari ya Ecknforde, Tanga, Tanzania kabla ya kujiunga na utumishi serikalini katika Ofisi ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kama Afisa Usalama wa Taifa. Hivi sasa, licha ya kuendelea na masomo yake ya Shahada ya Uzamifu (part-time) anajihusisha na ushauri wa kitaalamu katika masuala ya intelijensia na usalama (intelligence and security consulting), mikakati ya siasa (political strategy) na mahusiano na mawasiliano ya kimkakati (International PR and strategic communications), akiwa mwanzilishi na mmiliki wa kampuni ya ushauri wa kitaalam ya AdelPhil Consultancy iliyopo Glasgow, Uskochi.

> More about the Author

Recommended Books Arrow

Similar Books

Discussion - 23 comments

About Kbuuk

  • Our Story

    Inspired by the past and excited for the future, Kbuuk charges ahead.

  • Our Manifesto

    Kbuuk empowers authors worldwide. Come see what empowers us!

  • The Team

    Meet the Team. Find out who is behind every line of code.

Find out first:

Kbuuk Reader