Makala za Evarist Chahali Zilizovuma Magazetini

ISBN: 978-1-4769-8455-1

Category: Political,  Essays & Letters,  Africa,  Current Events

Keywords: Tanzania, Africa, Raia Mwema, Mtanzania, Kulikoni Ughaibuni, Chahali

Published: 03/28/2016

Views: 656

Words: 50,895

Rating:

Makala za Evarist Chahali Zilizovuma Magazetini

Toleo la Pili

By

Kitabu hiki ni toleo la pili la mfululizo wa vitabu vya mkusanyiko wa makala zangu katika magazeti mbali niliyowahi kuandikia au ninayoendelea kuandikia makala. Awali nilikuwa mwandishi wa makala katika gazeti la kila wiki la ‘Kulikoni,’ ambapo safu yangu ndiyo iliyozua jina la blogu yangu, yaani ‘Kulikoni Ughaibuni.’
Baadaye, nikaanza kuandika makala katika gazeti la ‘Mtanzania,’ na safu yangu iliitwa ‘Mtanzania Ughaibuni.’ Hatimaye, lilipoanzishwa gazeti la kila wiki la ‘Raia Mwema,’ nilijifunga nalo tangu mwanzoni, na safu yangu katika gazeti hilo linaloongoza nchini Tanzania yajulikana kama ‘Raia Mwema Ughaibuni.’
Kama ambavyo nimeshaandika mara kadhaa, mimi si mwandishi kitaaluma. Hata hivyo nimekuwa nikijihusisha na uandishi tangu mwaka 2008. Nilianza kuandika katika ‘gazeti la udaku’ la ‘Sanifu,’ kabla ya kuandikia gazeti jingine la ‘udaku’ la ‘Kasheshe’ na baadaye gazeti jingine la ‘udaku’ la Komesha.’ Katika magazeti yote hayo, nilikuwa naandika ‘unajimu wa utani,’ nikitumia jina la ‘Ustaadh Bonge.’ Jina hilo limeendelea kunikaa hadi leo kwa baadhi ya marafiki zangu.
Makala hizi zinahusu takriban kila mada, japo nyingi zazungumzia kuhusu siasa. Kimsingi, jina la ‘Kulikoni Ughaibuni’ lilitokana na swali nililokuwa ninajiuliza mara kwa mara baada ya kuja hapa Uingereza mara ya kwanza takriban miaka 14 iliyopita. Na swali hilo ni ‘kulikoni ugaibuni kuko hivi lakini kwetu kuko vile?’
Kwamba kwanini, kwa mfano, mara nyingi kwa hapa ukienda benki sio tu unaambiwa wewe mteja ni mfalme/malkia lakini pia huduma unayopewa yakufanya ujiskie hivyo bila hata kuambiwa. Hali ni tofauti sana huko nyumbani ambapo huduma nyingi hutolewa kama fadhila (privilege) badala ya haki/stahili kwa mteja.
Kingine kilichonisumbua sana katika kulinganisha niliyoshuhudia hapa na huko nyumbani ni suala la imani. Idadi kubwa ya wakazi wa hapa ni waumini wa dini yoyote. Na japo Uingereza ni taifa la Kikristo, idadi ya wasioenda kanisani wala kujitambulisha kama Wakristo ni kubwa kuliko wanaokwenda makanisani na kujitambulisha kama Wakristo. Kuna idadi kubwa tu ya makanisa
yaliyogeuzwa kuwa kumbi za starehe, hususan kutokana na ukosefu wa wahudhuriaji. Hata hivyo, licha ya ‘imani yao haba,’ uadilifu upo juu kwa kiasi kikubwa. Watu wengi hawaishi kwa kutegemea rushwa au ‘dili’ bali kujipatia kipato halali kwa njia halali.
Huko nyumbani, dini ni sehemu muhimu ya maisha yetu lakini cha kusikitisha kuwa pamoja na ushika-dini huo, maovu ni mengi mno ukilinganisha na hawa wenzetu ambao dini sio kitu cha muhimu sana kwao.
Uandishi wa makala zangu upo katika mfumo wa maongezi. Ninapoandika makala zangu hujiona kama ninafanya maongezi na wasomaji wangu. Na kimsingi, binafsi ninajitambulisha kama ‘mfanya maongezi’ (conversationalist). Japo kiwango changu cha elimu si haba, mara zote makala zangu zimekuwa zikimlenga mtu wa kawaida, awe profesa wa chuo kikuu au mtu aliyeishia darasa la saba, Mkurugenzi wa taasisi flani au ‘mama ntilie,’ mtu mzima au kijana…yaani ni kwa ajili ya watu wa kaliba zote.
Ni matumaini yangu kuwa makala hizi zitatimiza lengo langu kuu la uandishi, yaani kuhabarisha, kuelimisha, na kuburudisha. Mapungufu yoyote yaliyomo katika kitabu hiki ni yangu mwenyewe.

Kbook iPad Reader Makala za Evarist Chahali Zilizovuma Magazetini

Read it on any Device that supports ePub

Buy to read on eBook Tablet

$1.49

Kbook Mobile Reader

About the Author

Oct 04, 2015

Mwandishi wa kitabu hiki, Evarist Chahali, ni Mtanzania mwenye makazi yake jijini Glasgow, Uskochi, na anajitambulisha kama mwanaharakati wa mtandaoni (e-activitist) katika masuala ya haki za kijamii. Ni mhitimu wa Shahada ya kwanza katika Sosholojia (BA in Sociology) aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Shahada ya Uzamili katika Stadi za Vita (Master of Letters in War Studies) na Shahada ya Uzamili katika Utafiti wa Siasa (Master of Research in Political Research) alizopata katika Chuo Kikuu cha Aberdeen, Uskochi, ambapo bado anaendelea na Shahada ya Uzamifu katika Stadi za Siasa (PhD in Political Studies – Part-Time).
Kwa zaidi ya miaka 10, amekuwa akiandika makala katika magazeti mbalimbali nchini Tanzania, ambapo huko nyuma aliandikia magazeti ya ‘Kulikoni’ na ‘Mtanzania,’ na kwa sasa ni mwandishi wa makala katika gazeti la kila wiki linaloongoza nchini Tanzania, la ‘Raia Mwema. Kadhalika, mwandishi anamiliki blogu ya ‘Kulikoni Ughaibuni’ iliyoanzishwa mwaka 2006.

Awali, mwandishi alikuwa Mwalimu katika Shule ya Sekondari ya Ecknforde, Tanga, Tanzania kabla ya kujiunga na utumishi serikalini katika Ofisi ya Rais wa Jamhuri wa Munngano wa Tanzania. Hivi sasa, licha ya kuendelea na masomo yake ya Shahada ya Uzamifu (part-time) anajihusisha ushauri wa masuala ya ushauri wa kitaalamu (consulting) akiwa ni mwanzilishi na mmiliki wa kampuni ya ushauri wa kitaalamu ya AdelPhil Consultancy ya jijini Glasgow, Uingereza.

> More about the Author

Recommended Books Arrow

Similar Books

Discussion - 0 comment

About Kbuuk

  • Our Story

    Inspired by the past and excited for the future, Kbuuk charges ahead.

  • Our Manifesto

    Kbuuk empowers authors worldwide. Come see what empowers us!

  • The Team

    Meet the Team. Find out who is behind every line of code.

Find out first:

Kbuuk Reader